Wasamaria wema wakifanya utaratibu wa kumuokoa Dereva wa Gari aina ya Isuzu Trooper iliyopiga mweleka katika makutano ya Shule ya Msingi Oysterbay jijini Dar es salaam mara baada ya kugongana na gari nyingine aina ya Toyota Vitz iliyokuwa ikitokea upande wa Coco Beach mchana wa leo na kupekea dereva wa Gari hii (alikuwa ni Mama mtu mzima ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) kuumia sehemu ya kiuno na mkono.Gari hii ilikuwa inatokea upande wa St. Peter's kuelekea Morogoro Store na Vitz ilikuwa ikitokea upande wa bahari na kuvuka ghafla barabara hiyo.
Mashuhuda wakiwa wameizunguka gari hiyo mara baada ya kufanikiwa kumtoa Mama aliekuwa akiendesha Gari hilo.
Hivi ndivyo ilivyo hii Toyota Vitz baada ya kuhongana na Isuzu Trooper iliyopinduka.Picha na Mdau Pius Micky.
Oysterbay kuna mitaa yenye majina bana!
ReplyDeleteMakutano hayo yaliyopo jirani na Shule ya Msingi Oysterbay ni barabara za Haile Sellasie na Karume.