Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.) (wa kwanza toka kushoto) akimweleza jambo Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (wa tatu toka kushoto) wakati Baraza hili lilipotia saini makubaliano na kampuni hiyo kuendeleza ushirikiano katika kampeni za usalama barabarani ambazo Vodacom imekuwa ikidhamini tangu mwaka 2014. Akisikiliza pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga (wa pili toka kushoto). Tukio hilo lilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.) (wa kwanza toka kushoto) akishuhudia kutiwa saini kwa makubaliano ya kuendeleza ushirikiano katika kampeni za usalama barabarani baina ya Baraza hilo na kampuni ya simu za mikooni ya Vodacom Tanzania. Akitia saini kwa naiba ya Baraza ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga (wa pili toka kushoto) na kwa niaba ya Vodacom ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (wa tatu toka kushoto). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...