Kufuatia mkutano wa Watanzania waishio ujerumani na Rais wa Tanzania Mhe Jakaya Kikwete, Mweyekiti wa umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V Bw, Mfundo Peter Mfundo ameeleza matarajio ya Watanzania waishio Ujerumani.

Alifafanua kwamba japokuwa Rais Kikwete amebakiza muda mfupi katika uongozi wake lakini Umoja huo unaamini kuwa madam Rais Kikwete ameona umuhimu wa kufanya mkutano na Watanzania wanaoishi ujerumani basi anaweza akatekeleza mahitaji ya Watanzania hao.

Bw. Mfundo alifafanua pia hoja za msingi ambazo zitaibuka kwenye mkutano huo kuwa ni pamoja na Utekelezwaji wa upatikianaji wa fursa zilizopo Tanzania kwa watanzania wanaoishi Ujermani (Diaspora).

Aidha aliendelea kueleza kwamba hoja nyingine ya msingi ni kutaka kujua msimamo wa serikali juu ya Uraia Pacha, kwani Watanzania wanaoishi ujerumani wana kiu kubwa ya kujua swala la Uraia pacha limefikia wapi.

 akiendelea kuongea na Mtangazaji Grace Kabogo kupitia sauti ya Radio Deutsche Welle idhaa ya kiswahili Bw. Mfundo alisema kutokana na Vijana wengi wa Tanzania kujiajiri kupitia Muziki na kuupiga vita umasikini, Umoja wa Watanzania Ujerumani Utamuomba rais Kikwete kusaidia kupitisha msamaha wa kodi kwa Vyombo vya Muziki ili kuwawezesha Vijana wa Tanzania kumudu ununuzi wa vifaa hivyo, Bw. Mfundo alieleza moja ya changamoto wanazozipata ni pale umoja huo unapokosa mawasiliano ya moja kwa moja na Idara ya Diaspora Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...