Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika sherehe ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015. sherehe hiyo imefanyika Januari 9, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(wa tatu kushoto) atoe hotuba yake (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Bw. Daud Msangi(wa pili kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa tatu kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw. Dickson Mwaimu(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa) .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...