Sikukuu ya Maulid kitaifa inaratajia kufanyika wilayani
Korogwe mkoani Tanga Januari 4 Mwaka huu.
Kwa taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na
kusainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (Bakwata),Suleiman
Said Lolila ilisema Maulid itaanza Januari 3 na kumalizika Januari 4.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania ,Issa Bin Shaaban Simba anawatakia waislaam na
wananchi kwa ujumla maulid njema.
Hata hiyo Katibu Mkuu Lolila aliwataka waislam wote nchini
kushirikia kikamilifu katika mazazi ya M.tume mohamad (S. AW)
Wabillah Tawfiq.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...