Na Anitha Jonas - MAELEZO.
SERIKALI
imedhamiria kupunguza msongamano wa magari ndani ya jiji la Dar es Salaam kwakujenga
barabara sita zitakazo ambazo ujenzi wake utasimamiwa na TANROADS. Ujenzi
huo unatarajiwa kugharimu sh. trilioni moja ambapo lengo barabara hizo ni kupunguza adha ya msongamano wa magari katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es
saalam.
Waziri
wa Ujenzi Dkt.John Magufuli alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akiweka jiwe la
msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara hizo. “Barabara
hizi zinajenga kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
asilimia 100 na lengo kubwa la mradi huu ni kupunguza msongamano ndani ya jiji”
alisema Magufuli.
Magufuli
aliendelea kusema “Rai yangu kwa Watanzania
wote ikiwemo madereva wa magari yenye uzito mkubwa kuacha kupita barabara zisizo stahimili uzito
wa magari hayo na kuwaasa wananchi wa maeneo jirani waache kugeuza
barabara hizo kuwa maduka au fremu za biashara”.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Said Mecky Sadick aliwaasa wananchi wa Dar es
Salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali na wakandarasi pale watakapoombwa
wasogee nje ya barabara ili kufanikisha
ujenzi huo kwani barabara ni sehemu ya maendeleo na ni vyema kila mmoja kuwa
mzalendo na kuacha itikadi za vyama .
“Nikiwa
kama mdau mkubwa wa maendeleo ya jiji la Dar es Salaam nitahakikisha
wakandarasi hawa wanamaliza kazi ya ujenzi huu
kwa wakati na nitakuwa nikiwafuatilia kwa karibu katika kuhakikisha viwango
vinazingatiwa ili barabara hizi
ziweze kuwa mkombozi wa tatizo la msongamano katika jiji,” alisema Sadick.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu Wakala wa Usimamizi
wa Barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick
Mfugale alizitaja barabara zinazotarajiwa kuanza kujengwa katika mradi wa
kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam ni Ubungo Msewe
hadi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 2.6, Ubungo Externo
hadi Kilungule kilomita 3, Kigogo hadi Tabata Dampo kilomita 1.6.
Mfugale
alisema kuwa barabara nyingine ni Kinyerezi hadi Kifuru kilomita 4 kwa awamu ya
kwanza na badae ni Kifuru hadi Maramba Mawili kilomita 10, pamoja na Mbezi Mwisho
hadi Goba Tangi Bovu ambayo ni kilomita 20.
Katika
Ziara hiyo ya kuweka jiwe la msingi Waziri Magufuli aliambatana na watendaji na
viongozi wa TANROADS, wabunge wa maeneo hayo, watendaji wa wizara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...