Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anatarajia kuyafutia usajili zaidi ya Mashirika 1000 kutokana na kutotimiza matakwa ya kisheria katika utendaji kazi wake tangu yasajiliwe.

 Hatua hiyo inatokana na maelekezo ya Bodi ya Uratibu ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kikao chake kilichofanyika hivi karibuni mkoani Geita. 

Kufutwa kwa mashirika tajwa kunatokana na kushindwa kutoa taarifa zake za kila mwaka kama inavyosisitizwa na sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, 2002 hali inayosababisha kazi za mashirika hayo kutofahamika vyema na hivyo kukosa sifa ya kuendelea kufanya kazi kwa mujibu wa sheria. 

Orodha ya Mashirika tajwa itatolewa kwa umma hivi karibuni na inahusisha pia Mashirika ya Kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...