Afisa Mtendaji Mkuu Dr Kamugisha Kazaura atembelea mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Mbeya ikiwa na lengo la kukagua miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa TTCL wa mikoa hiyo.

Dr Kazaura ailijionea juhudi mbalimbali zinazofanywa na wafanyakazi wa TTCL katika kuhakikisha miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inakuwa salama muda.

Hivi sasa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imekuwa kampuni pekee ya mawasiliano ambayo imefanikiwa kuunganisha wateja mbalimbali kupitia mtandao wake.

Wateja hao ni pamoja na TAMISEMI, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mabenki, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali (CAG),Wizara ya Fedha, watoa huduma za mtandao/intaneti (ISPs) pamoja Makampuni ya Simu

Pia TTCL imefanikiwa kuunganisha nchi jirani katika ukanda huu wa afrika Mashariki (Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda) pamoja na nchi za kusini wa Jangwa la Sahara (SADC) ambazo ni Malawi na Zambia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua mitambo ya TTCL mkoani Lindi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akipokea maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa TTCL Mtwara kuhusu juhudi zinazofanyika kulinda na kusimamia mitambo yake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua Mtambo wa Mkongo wa Taifa, pembeni yake ni Mkuu wa Idara ya Ufundi wa TTCL,Senzige Kisenge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...