Mwishoni mwa wiki iliyopita vijana machachari wa Yamoto Band walifanya ziara maalum kutembelea ubalozi wetu a jijini London, Uingereza, na kupata fursa ya kukutana na Balozi Peter Kallaghe na kujadili nae kuhusu tasnia ya muziki Tanzania. Aidha Mh Balozi Kallaghe aliwapongeza kwa kazi zao nzuri na kuwaasa kuwa waendelee kujituma kwa moyo zaidi, huku akiwatahadharisha wasilewe sifa na kuwa nguvu ya soda, bali wawe mfano wa kuigwa kwa kudumu pamoja kwa muda mrefu. Bendi ya Yamoto iko nchini Uingereza kwa ajili ya kufanya maonyesho maalum.
 Mh Balozi Kallaghe akiongea na vijana wa Yamoto Band katika ubalozi wa Tanzania jijini London
 Mh Balozi Kallaghe akipata picha ya kumbukumbu na  vijana wa Yamoto Band 
Promota wa safari ya Yamoto Band jijini London, Jestina George, akiwatambulisha Yamoto Band kwa balozi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. jamani jamani huyo coordinator, alishindwa kuwaambia hao watoto dress code za kwenye ofisi kama hizo, hivi hawawaoni wenzao kina JAy Z, wanavaa kutokana na sehemu, badilikeni bana, hasa nyie mnaojiita mameneja.

    ReplyDelete

  2. Wanamuziki wetu na 'The called Bongo Super Stars, hebu jaribuni kuvaa mavazi kuendana na mahali mnapokwenda au mtu mnayekutana nae, Ofisi za Serikali zina heshima yake jamani. Kwani kingeharibika nini iwapo mngevaa vizuri tu achana na jeans mchano au pensi. Coordinator vip hata kuwashauri vijana? Mbona wewe umevaa rasmi?

    ReplyDelete
  3. Wameharibu, dad Jestina umeshindwa kuwaambia vijana waulambe?

    ReplyDelete
  4. Niliishiwa maneno ya kuongea..kuona mtu anaona ufahari kuvaa ki-jinsi kimechanika kwenye goti ilhali yuko katika ofisi nyeti...siyo kosa lao ila ni coordinator au huyo meneja wao. ndo maana bado watu wana relate muziki na uhuni kumbe wachache ndo wanaharibu. Tubadilike!

    ReplyDelete
  5. Jestina hebu toa hiyo vitoto tupa huko nje mnali kabisa,hawajui hata kuvaa,kwani hamuwafundishi?au nyie mkiwageuza punda basi mnaridhika.Fundisha kuvaa nguo.
    Punda=kuwabebesha kamzigo.

    ReplyDelete
  6. Kuvaa wanajua vijana wa usasa, ama sivyo. Lakini hawajui mavazi ya kujikinga na baridi. Ulaya sasa baridi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...