Home
Unlabelled
CHAMA CHA ALBINO TANZANIA CHATOA TAMKO JUU YA HALI YA MAUAJI YA ALBINO NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ni kweli kabisa, tangu Albino waanze kuuawa sijawahi sikia Mheshimiwa Rais akiongea kitu sasa mie sijui kwamba anawatumia viongozi wengine au.
ReplyDeleteHii ni dhambi kubwa sana sana, kama ni kweli wakati huu wa kampeni za uchaguzi ndo mambo haya yanatokea, this is too bad, ninalaani kabisa kitendo hiki na niko tayari kufanya maombi ili siku moja wafahamike hawa wenye biashara haramu ya ngozi na viungo vya binadamu. Naamini Mungu wangu atanisikiliza. One day hili litakuwa wazi na wahusika wataaibika sana sana.
ReplyDeleteWatanzania wenzangu ninajivunia sana kuzaliwa Tanzania, na kwa hakika naipenda sana nchi yangu. Lakini vitendo vya Watanzania wenzetu wachache wenye roho za aina yao, siwapendi. Kwanini wawaue Watanzania wenzao? Kuua ni kitu kibaya sio kwa kumwua Mtanzania tu hata kumuua binadamu mwingine yeyote duniani.
ReplyDeleteKibaya zaidi Tanzania, kubagua watu na kuwaua kwa imani zao za ajabu. Mtu anadiriki hadi kumwua mtoto mdogo mwenye albino, inauma kuliko kiasi.
Serikali yetu inafanya nini kukomesha unyama huu? Miaka ya 1971 alipouliwa Dr Kleruu, hukumu ya Mwamwindi ilikwenda fasta na alinyongwa. Vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto wa shule iliyomkabili Babu Seya ilipelekwa fasta na kutolewa hukumu ya jela ya maisha kwa watuhumiwa. Francis Choka kapiga mtu, kesi imepelekwa fasta mtuhumiwa kahukumiwa miaka mitatu. Swali, ni kesi ipi ya watuhumiwa wa mauaji wa albino tumesikia maendeleo ya kazi zao na kutolewa hukumu zao?
Serikali na vyombo vyake vyote vya sheria. Mimi na wenzangu wanaoniunga mkono, tumechoshwa na matendo yenu ya kutufanya sisi vipofu, viziwi na mabubu.
Sasa tunataka kuona, kusikia na tutamke kama walivyotoa tamko lao "ALBINO"
Mdau
Hii inasikitisha sana mtu anatoa roho ya mwenzake kisa pesa au ushirikina wa kufanikiwa katika maisha. Tafadhanli serikali iweke kipaumbele kwenye swala hili. Kutoa elimu kwa jamii tukianzia na maeneo yaliyoadhirika zaidi. Albino ni binadamu kama sisi tofauti ni rangi ya ngozi yao tu.
ReplyDeleteMungu tufungue manake tuko kwenye giza nene.
mdau wa pili nakubaliana na wewe kwamba uchaguzi unakuja ndo mambo haya yamezidi kushamiri...kwa sababu wateja wakuu wa hivyo viungo ni hao hao tuliowakabidhi majukumu ya kutulinda..
ReplyDeletepoleni wote wahanga wa hili..
hadi roho inaniuma kwa jambo hili ..
mungu atusamehe