Mwenyekiti
wa Chama cha Kutetea Abiria Taifa(Chakua),Hassan Mhanjama akionyesha
barua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) ambazo wamejibiwa na
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) katika
Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es Salaam.(Picha na
Emmanuel Massaka).
Na Chalila
Kibuda.
Chama Cha
Kutetea Abiria (Chakua) kimesema kuwa kutokana na bei ya mafuta kushuka nchini
nauli ya daladala na nauli ya mabasi mikoani inatakiwa kushuka kwa asilimia 25.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo,Mwenyekiti wa chama hicho,Hassan Mhanjama amesema
Mamlaka ya Usafiri wa Maji na Nchi Kavu (Sumatra) ina wajibu wa kuitisha
mkutano na wadau kujadili kushuka kwa gharama ya nauli ili mwananchi aweze
kunufaika bei ya kushuka kwa mafuta.
Mhanjama
amesema kwa nauli ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Kilomita 10 ya sh.400 inatakikwa
kushuka na kufikia sh.300 na nauli ya mkoani ya Sh.40,000 inatakiwa kushuka na
kufikia sh.30,000.
Amesema kuwa
wamiliki wa Daladala na mabasi ya mikoani kusema bei ya vipuli na tairi
zimepanda haihusiani na kushuka kwa bei ya mafuta kwani wakati mafuta yanapanda
wanalamika na bei kupandisha hivyo sasa wanalazimika kushusha nauli zao.
Serikali inabidi iwe na hurumna na wananchi wake.Ni dhahri kuwa wakati bei zinapanda factor kubwa na iliyokuwa wazi ni bei ya mafuta lakini wakati wa kutakiwa kushuka kwa bei inakuja na mlolongo wa sababu mara vipuri nk sasa sijui wadau tushike lipi.
ReplyDelete