Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA, kimetaja makundi ya timu zitakazoshiriki kucheza hatua ya 18 bora (hatua ya pili) ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam,inayotarajia kuanza kutimua vumbi mapema mwezi huu.
Katika kundi 
(A) limepangwa kuwa na timu za Simba U20,Red Coast,Sifa UTD,Shababi,Ukonga UTD,Zakhem,Ugimbi,Beirahotspurs na Pan Africa.
Katika kundi 
(B) litakuwa na timu za Yanga U20,Stakishari,FFU,New Kunduchi,Sinza Stars,Changanyikeni,Tuamoyo,Sifapilitan na Azania Unga.

Ligi hiyo ya mkoa wa Dar es salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36, imeingia katika hatua ya pili,ambayo  itaanza Februari 11 mwaka huu katika viwanja mbalimbali.
Kundi (A)
 Simba U20    vs    Red Coast       (Karume)
Sifa UTD         vs   Shababi           (Mwl/Nyerere)
Ukonga UTD  vs   Zakhem           (Airwing)
Ugimbi           vs   Beirahospurs  (Bandari)

KATIKA KUNDI (B) Februari 12
Yanga U20    vs   Stakishari          (Karume)
FFU                vs  New Kunduchi   (Benjamini Mkapa)
Sinza Stars    vs  Changanyikeni   (Kines)
Tuamoyo      vs  Sifapolitan          (Bandari)
Viongozi wa DRFA bado wanatoa wito kwa viongozi wa vilabu mbalimbali,mashabiki na wakazi wa jiji pamoja na maeneo ya jirani,kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya wachezaji.
 Imetolewa na DRFA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...