Mfuko wa Pensheni wa GEPF umesaini mkataba wa uwekezaji na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) katika eneo la Bunju. Uwekezaji huo utakaohusisha kumbi za mikutano (Conference Halls) zenye uwezo wa kuchukua watu Zaidi ya 1,200, migahawa (Restaurants), Hoteli yenye hadhi ya kimataifa yenye vyumba Zaidi ya 102, Maktaba, Bwawa la kuogelea (Swimming Pool) pamoja na sehemu za mazoezi (Gymnasium) Uwekezaji huo utagharimu Zaidi ya shilingi Bilioni 33 za kitanzania na unategemewa kukamilika katikati ya mwaka huu 2015.
Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud Msangi (wa pili kulia) akiongoza majadiliano ya awali kati ya Menejimenti ya GEPF pamoja na Menejimenti ya NBAA kabla ya zoezi la kutiliana saini mkataba wa uwekezaji.
Mwenyekiti wa Bodi ya GEPF,Bi. Joyce Shaidi (kulia) pamoja na mwenyekiti wa NBAA Profesa Issaya Jairo wakisaini mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji wa pamoja wakiongozwa na mwanasheria wa NBAA Bi Agness Kessy.
Utiaji saini huo ulishuhudiwa na makamu mwenyekiti wa NBAA Bi Anna Mbughuni ( mwenye suti ya blue), Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Bw Pius Maneno, Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Bw Daud Msangi pamoja na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GEPF Bw Festo Fute.
Mwenyekiti wa Bodi ya GEPF Bi Joyce Shaidi akibadilishana nyaraka za mkataba wa uwekezaji wa pamoja na Mwenyekiti wa NBAA Profesa Issaya Jairo.
Pichani baadhi ya watendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) wakifurahia jambo mara baada ya zoezi hilo kukamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...