HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO
WA 18 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAREHE 7 FEBRUARI, 2015
I: UTANGULIZI
(a)
Masuala ya
jumla
Mheshimiwa
Spika,
1.
Tumekuwepo hapa kwa takriban siku 12 katika
shughuli za Mkutano wa 18 wa Bunge lako Tukufu. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi
Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.
2.
Lakini tumekutana hapa tukiwa tumeshuhudia
mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na Wenyeviti wa baadhi ya Kamati za Kudumu
za Bunge. Niruhusu nitumie nafasi hii ya awali kuwapongeza Mawaziri na Naibu
Mawaziri wote ambao wameteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali katika mabadiliko
hayo. Aidha, napenda niwapongeze Wenyeviti watatu pamoja na Makamu mmoja kwa kuchaguliwa
kuongoza Kamati za Kudumu za Bunge ikiwemo Kamati ya Bajeti, Kamati ya Nishati
na Madini na Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala. Tunawatakia afya njema Mawaziri,
Naibu Mawaziri na Wenyeviti wote katika kutekeleza majukumu yao mapya.
Mheshimiwa Spika,
3.
Tangu tulipomaliza Mkutano wa 16 na 17 wa
Bunge lako Tukufu, kumetokea majanga katika sehemu mbalimbali Nchini ikiwemo
mafuriko na mapigano ya Wakulima na Wafugaji kule Morogoro, pamoja na ajali za
barabarani. Naomba nitumie nafasi hii kuwapa pole wote walioathirika na majanga,
maafa na ajali za barabarani. Kwa wale
waliopoteza maisha tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala
pema peponi Amina.
b) Maswali
Mheshimiwa
Spika,
4.
Katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kuuliza maswali ya
kawaida na yale ya papo papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Jumla ya maswali 122 ya msingi na 313 ya nyongeza yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na
Serikali. Aidha, Maswali 15 ya msingi na 13 ya nyongeza yaliulizwa na kujibiwa kwa utaratibu wa maswali ya papo
kwa papo kwa Waziri Mkuu.
(c) Miswada
na Taarifa Mbalimbali
Mheshimiwa
Spika,
5.
Tunahitimisha
Mkutano huu tukiwa tumekamilisha kazi kubwa ya kusoma na kujadili taarifa mbalimbli
za Kamati za Bunge za Kisekta na zisizo za Kisekta. Kamati za Kisekta ambazo
Taarifa zake zimewasilishwa na kujadiliwa na Waheshimiwa Wabunge ni zifuatazo:
i)
Kamati ya Miundombinu;
ii)
Kamati ya Nishati na Madini;
iii)
Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira;
iv)
Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji;
v)
Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala;
vi)
Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa;
vii)
Kamati ya Masuala ya UKIMWI;
viii)
Kamati ya Ulinzi na Usalama;
ix)
Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa;
x)
Kamati ya Huduma na Jamii; na
xi)
Kamati ya Maendeleo ya Jamii.
6.
Aidha, Bunge Lako Tukufu lilipokea na
kujadili Taarifa za Kamati zisizo za Kisekta zinazosimamia Fedha za Umma
zifuatazo:
i)
Kamati ya Hesabu za Serikali;
ii)
Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa; na
iii)
Kamati za Bajeti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...