Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumzana na Kamati Kuu ya
Chama Cha SPLM ambapo alipeleka ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,kikao hicho kilikuwa
chini ya Mwenyekiti wa chama cha SPLM ambaye pia ni Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir, Ikulu mjini Juba.
Mwenyekiti wa chama cha SPLM ambaye pia ni Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ambacho Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihudhuria.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Rais wa Sudan ya Kusini Rais
Salva Kiir mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu cha chama
cha SPLM ,kikao hicho kilimalizika usiku wa manane mjini Juba ,Sudan.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha Kamati Kuu ya chama cha
SPLM mjini Juba,kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa SPLM ambaye pia ni
Makamu wa Rais wa nchi hiyo James Wani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...