Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa  kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam,Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini  (NECTA),Dk.Charles Msonde amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu umeongezeka  kwa asilimia 12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Katika matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab ,Nyakaho I. Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia wavulana.

Shule za Sekondari za St.Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi nane na kufanya shule hizo kuingia katika 10 bora kwa kutoa idadi wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule zingine.

Msonde amasema matokeo hayo  yanatokana na mfumo mpya  wa GPA kwa kuangalia masomo saba  hivyo ufaulu umetokana na mfumo huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini,Dk. Charles Msonde akizungumza na wanahabari jijini dar leo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...