Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Mkuranga,Benjamini Majoya akipokea msaada  uliotolewa na Kampuni ya Upendo Media Group,Benki ya Maendeleo na Fifa Flow Limited kwa  Mteule Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani,Chediel Luiza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya Azania Front Jijini Dar es Salaam. 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.


AFISA Elimu Sekondari,Wilaya ya Mkuranga Benjamini Majoya amekishukuru Kituo cha Radio cha Upendo pamoja na gazeti la Upendo kwa kutoa habari za Wilaya ya Mkuranga na kupata msaada wa madawati pamoja na sare za shule kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Majoya ametoa shukrani hizo wakati akikabidhiwa madawati 40 na sare kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu iliyofanyika leo katika viwanja vya Azania Front jijini Dar es Salaam.

Madawati na sare kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu zimetolewa na Benki ya Maendeleo ,Kampuni Fifa Flow Limited pamoja na Kituo cha Radio Upendo pamoja gazeti la upendo.

Msaada huo umetokana na Kituo cha Radio Upendo pamoja gazeti la upendo kwenda katika Wilaya ya Mkuranga kutafuta habari na kuona kuna umuhimu wa kupata msaada wa madawati pamoja sare kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Maendeleo, Ibrahimu Mwangaraba amesema wanatambua umuhimu kama benki kuwa wanaowasaidia watakuwa ni wateja wa benki yao,wengine ni viongozi mbalimbali ambao watasaidia maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...