
Meneja
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua
jambo kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani), wakati wa hafla
fupi ya uzinduzi wa king'amuziki kipya cha DStv HD leo jijini Dar.
Kulia ni kwake ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald
Shelukindo na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha
Samalu.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Andrew Chale
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo imezindua king’amuzi kipya cha DStv HD
ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza hapa Nchini. Akizungumza
na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Meneja
Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu
wa huduma hizo alisema king’amuzi hicho kina ubora wa hali ya juu
ikiwemo kuonyesha picha zenye ubora mzuri zaidi.
Pia alieleza kuwa, DStv HD
mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu
cha sauti Dolby Digital 5.1. “Wateja wa DStv watafurahia ving’amuzi hivi
kwa ubora wa hali ya juu hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa kwani
ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania” alisema Ronald Shelukindo.
Meneja
uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora
wa king'amuzi hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa
habari leo jijini Dar.
Ronald
Shelukindo akielezea kwa kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia
vipindi mbalimbali ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa
kupendekeza atazame kipi gani, muda gani na wakati gani?.
King’amuzi cha “DStv HD,
mteja anaweza kujipangia atazame kipindi gani ama kwa wakati autakao
yeye, ambapo anachoweza ni kuseti hicho kipindi akipendacho na kisha
anaweza kukiangalia kwa wakati wake, hata kama muda umepita kwa wakati
huo kinarushwa kwenye chaneli husika” alifafanua Ronald Shelukindo.
Kwa
upande wake, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu
aliwahimiza watanzania kuchangamkia vinga’muzi hivyo vya DStv HD,
ambavyo kwa sasa vipo karibu maduka yote ya Mawakala wa DStv, kwa bei
rahisi kabisa vikiwa vinapatikana kwa sh 99,000/ kwa mteja mpya huku kwa
wateja walio na ving’amuzi vya zamani vya DStv watakaotaka
kubadilishiwa, watalipia sh 39,000/ tu.
Meneja
uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha
king'amuzi kipya cha DStv HD kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...