Benki ya NMB imewafagilia jeshi la polisi kwa kuikubali benki yao kuwa benki chaguo la kwanza na kusema kitendo hicho kinadhihirisha kuridhishwa kwao na huduma bora za kibenki zinazotolewa na NMB kupitia Makundi mbalimbali katika jamii ya Tanzania.
Hayo yalisemwa jana mjini Dodoma na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Tom Borghols alipokuwa akitoa Maneno ya utangulizi.
Aliyasema hayo kabla ya Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi wa benki ya NMB - Abdulmajid Nsekela kuwasilisha maada juu ya mchango wa taasisi za kifedha katika shughuli za polisi.
NMB ndiyo benki pekee ambayo imekuwa ikidhamini Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Polisi unaofanyika kila mwaka
Jeshi la polisilimeipongeza benki ya NMB kwa udhamamini huo na kuiomba iendelee kuwasaidia pale wanapokwama kwani kufanya hivyo ni kuunga juhudi za jeshi la polisi kusimamia sheria za nchi na kuzuia uhalifu katika jamii ambayo ndani yake kuna wateja wa NMB.
NMB imedhamini kiasi cha shilingi Milioni 75 kwaajili ya maandalizi na shughuli za mkutano pamoja na kutoa pikipiki 5 zenye thamani ya shilingi Milioni 10 kwaajili ya kurahisisha kazi za operation za polisi za kila siku.
NMB ndiyo benki yenye mtandao mkubwa Zaidi nchini ukiwa na matawi Zaidi ya 75 na ATM Zaidi ya 600 nchi nzima pamoja na Zaidi ya wateja Milioni 2, hazina ambayo hakuna benki nyingine nchini yenye nayo
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bw. Tom Borghols akitoa Maneno ya utangulizi kwenye mkutano wake na maafisa waandamizi wa jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam
Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi wa benki ya NMB Bw. Abdulmajid Nsekela kuwasilisha mada juu ya mchango wa taasisi za kifedha katika shughuli za polisi kwenye mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathia Chikawe (mwenye suti katikati mbele) akiwa na maafisa wa polisi waandamizi katika picha ya pamoja na maafisa wa Benki ya NMB
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...