Na Chalila Kibuda.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezuia
maandamano ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF) na
kusema watakaoandamana
kesho nguvu ya dola itatumika
Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamanda wa
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP),Suleiman Kova amesema wamewashauri vijana hao na kusema wataandamana hivyo
ni lazima nguvu itumike kuzima maandamano hayo kutokana na kuzuia kufanyika kwa
shughuli zingine.
Kova amesema kusudi la maandamano hayo ni ukiukaji wa haki za binadamu kwa jeshi la polisi pamoja na Tume ya Uchaguzi kuongeza siku
za kuandikisha kutoka siku saba hadi 14, ambapo waliwashauri kwenda huko kwa viongozi lakini wameshindwa kufanya hivyo na
kuwataka wakate rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ili wafanye maandamano, nalo
wamekataa.
“Mambo haya yote yakutaka kufanya maandamano
yanazungumzika lakini wanataka kufanya hivyo ni lazima nguvu itumike kuzima
kuacha kila mtu anafanya kitu anachotaka ni kufanya nchi isitawalike na sisi
tunafanya nchi itawalike kwa watu kufuata taratibu”amesema Kamishina Kova.
Amesema kuwa Jeshi la Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa
kesho wamejipanga katika kuhakikisha maandamano ya vijana hao hayafanyiki na
watakaothubutu nguvu ya polisi itakuwa juu yao .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...