Ndugu, Issa Wahichinenda
Mkurugenzi wa uendeshaji wa UTT AMIS akitoa maada kuhusiana na fursa za
uwekezaji katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja kwa wafanyakazi wa ofisi ya
Mkaguzi wa hesabu za serikali katika kikao cha baraza la wafanyakazi kilicho
fanyika hivi karibuni Mtwara.
UTT AMIS ndiyo magwiji katika kuanzisha na kuendesha Mifuko
ya Uwekezaji wa Pamoja (Mutual Funds) hapa nchini. Mpaka sasa UTT AMIS
inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha,
Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya
Shilingi bilioni 235.
Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety,
Liquidity and Returns). Mifuko hii inayoendeshwa na UTT AMIS ni kwa ajili ya watanzania wote, vikundi,
Saccos, taasisi, kampuni na mifuko ya hifadhi za jamii. Wawekezaji wote
wananufaika kwa kupata faida shindani,
uwekezaji mseto ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu
wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya vipande vya mifuko hutangazwa
kila siku za kazi.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha baraza la wafanyakazi la
ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali wakifuatilia uwasilishwaji mada
kuhusiana na fursa za uwekezaji katika mifuko ya Pamoja inayoendeshwa na UTT
AMIS.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...