Mhe.Liberatus Mulamula

Balozi wa Muungano ya Jamhuri ya Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberatus Mulamula, alipozungumza  katika kongamano  la mapambano dhidi ya gojwa la saratani duniani, aliwataka wanaDiaspora wa nchi za kiAfrika kuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na watalaamu wa vitengo vya afya duniani ili kuboresha upatikana wa huduma za afya barani Afrika. Mhe. Balozi Mulamula, ambaye pia ndie aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo alizungumzia faida za kutumia Teknolojia  ili kuboresha mawasiliano kati ya wataalam, utafiti na  elimu . 
Nia mojawapo ya  kongamano la Global Health Catalyst Cancer Summit 2015 ni kuboresha huduma mahiri za saratani barani Afrika kwa  kutumia ( Information and Communication Technologies (ICTs);Teknolojia ya mawasiliano kati ya wataalam wa gojwa la saratani wa nchi za nchi za ng'ambo  na wataalam waliopo barani Afrika.Mhe. Balozi L. Mulamula, alikabidhi Tunzo Maalum kwa Bigwa wa Tiba ya Saraatani Dr. Twalibu Ngoma. Dr.Ngoma ni miongoni mwa wataalam wa kuigwa ambaye amepata elimu ya juu nje ya nchi na kureja nyumbani ili kuboresha upatikanaji wa huduma na elimu ya saratani nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...