Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza siku ya Jumanne, wakati wa uzinduzi wa ripoti mpya kuhusu mkakati wa kimataifa wa kila mwanamke, kila mtoto ambao Ban Ki Moon aliuanzisha mwaka 2010.  Ripoti hiyo inaonyesha kuwa vuguvugu hilo ambalo kwa ushirikiano baina ya wadau mbalimbali zikiwamo serikali, mashirika ya kimataifa, asasi zisizo za kiserikali, wasomi, wanaharakati na sekta binafsi zimewezesha kuokoa maisha ya wanawake na watoto 2.4 milioni.
katika picha hii ya maktaba wanaonekana Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu Ban Ki Moon, wakifurahia jambo walipokuta katika moja ya mikutano ya kimataifa. Akielezea nini kilichosababaisha vuguvugu hilo la kila mwanamke, kila mtoto kuwa na mafanikio makubwa.Ban Ki Moon alisema utashi wa kisiasa na utayari ulioonyeshwa na viongozi mbalimbali akiwamo Rais Jakaya Kikwete ndio baadhi ya sababu zilizochangia kufanikiwa kwa mkakati huo. Rais Kikwete akiwa mwenyekiti mwenza na Waziri Mkuu wa Canada walisimamia Kamisheni ya Habari na Uwajibikaji baada ya kuombwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, jukumu ambalo wamelitekeleza kwa ukamilifu na kutoa mchango mkubwa katika uboreshaji wa afya ya mama na mtoto kupitia vuguvugu hilo la kila mwanamke, kila mtoto.

Na Mwandishi Maalum.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban ki Moon,  amesema kama si utashi wa kisiasa,  kujituma, na kujitolea kulikofanywa na  viongozi mbalimbali aliowaomba kufanya naye kazi kwa karibu huku wengine wakijitolea wenyewe,  uhai wa  wanawake na watoto  2.4 milioni  usingeokolewa.

Ban Ki Moon ameyasema hayo siku ya  Jummane wakati wa uzinduzi wa  ripoti mpya  kuhusu mkakati wa kimataifa kuhusu vuguvugu la  kila  mwananamke, kile mtoto, ( every woman, every child) mkakati ambao Ban Ki Moon  aliuratibu mwaka 2010 .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...