Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Matosa Kimara jijini Dar es Salaam, Rabisante Lema akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kukabidhi hundi ya sh. milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu ya kanisa hilo wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa. Jumla ya shilingi milioni 50 zilipatikana katika harambee hiyo. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akimkabidhi hundi ya sh. millioni kumi Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Matosa Kimara jijini Dar es Salaam, Mhandisi Simon Kihunzi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kanisa hilo, wakati wa harambee iliyofanyika kanisani hapo, ambapo jumla ya shillingi milioni 50 zilipatikana. 
Godwin Semunyu akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charls Kimei baada ya kutoa mchango wake. Kulia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Rabisante Lema.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi hii Benki ya Kanisa? mbona hatusikii hata siku moja imetoa msaada wa kujenga japo madrasa achilia mbali msikiti! maana this is too much now! hivi ingekuwa inajengwa misikiti kelele zake ingekuwaje unajua INATIA UCHUNGU!

    ReplyDelete
  2. Hizi jazba za mdau wa kwanza ndiyo zinachochea udini..

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu hizo pesa ni zinatokana na riba. Hivyo haziwafai.

    ReplyDelete
  4. We Mdau wa kwanza ondokana na Ujinga huo!..

    ReplyDelete
  5. Angalieni Video ya Mzee mmoja alikuwa anaitwa JK Nyerere ambae Mungu alitupendelea sana kwa kutuletea Watanzania mtu mwenye akili sana na mwenye kuweza kuona mbali.

    Watanzania hacheni UDINI, UKABILA na zidisheni nguvu kulifanya Taifa ili la Tanzania kuwa Taifa lenye nguvu duniani, Afrika na Vizazi vyetu viwe na Urithi mwema hapo baadae.

    Video https://www.youtube.com/watch?v=WYD_ewe1zJE

    https://www.youtube.com/results?search_query=nyerere

    ReplyDelete
  6. Dhu mdauwa tatu , ulicho sema , kweli hiyo akili . Lakini viwanda vya pombe kama sijakosea havifanyi hivyo ! Hesabu ndogo tu , kwani akisaidia hospitali wanaotipiwa ni kinanani ! Kutotumia akili kwenye vitu vidogo vidogo matokeo yake watu wakisema kama mdau wa kwanza , majibu yenu mnayajua . Kweli kusoma sana sio kuelimika!

    ReplyDelete
  7. Pengne ni pesa zake za mchango binafsi siyo za ofisi kama iliyoandikwa hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...