BONDIA IBRAHIMU CLASS "King Class Mawe" mwenye rekodi namba moja nchini Tanzania na ni namba 216 kwa Dunia  amepoteza mpambano wake wa kwanza nchini Namibia kwa kupigwa kwa pointi na bondia Julius Indongo mwenye rekodi ya Namibia namba moja na Duniani ni namba 76 kwa ubora

mpambano huo uliofanyika machi 20,mwaka huu katika ukumbi wa Windhoek Country Club Resort,Windhoek, Namibia.

Mpambano huo ulianza kwa kasi ya ajabu ambapo bondia Class alimkalisha chini Indongo na kuhesabiwa na mpambano kuendelea kwa mashambulizi ya zamu kwa zamu kila upande,hata hivyo mpaka mwisho wa mchezo Class alipoteza mpambano uho kwa point.

mpambano huo ni wa pili kwa Class kucheza nje ya nchi baada ya ule wa kwanza kupigana nchini Zambia mwaka jana na kurudi na ubingwa wa WPBF Africa.

Kabla ya kuchaguliwa kwenda kupigana nchini Namibia,Class alimdunda bondia Cosmas Cheka na kunyakuwa mkanda wa U.B.O Africa na kumfanya amiliki mikanda miwili ya Africa mpaka sasa. 

Mpambano huo anaupoteza baada ya miaka mitano iliyopita kuwapiga mabondia mbalimbali, Class ananolewa na jopo la makocha linalongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta',Kondo Nassoro pamoja na Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye humpa ushauli anapokuwa ulingoni jinsi ya kukabiliana na mpinzani anaecheza nae.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...