Bondia Mohamed Matumla atapanda ulingoni kuzichapa kuwania ubingwa wa dunia wa WBF Machi 27 dhidi ya Wang Xin Hua wa China.

Pambano hilo la raundi 12 la uzani wa Bantam limepangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa pia na bingwa wa zamani wa dunia wa uzani wa juu, Francois Botha.

Promota wa pambano hilo, Jay Msangi alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na pambano litasimamiwa na Shirikisho la ngumi la dunia la WBF ambaye rais wake atawasili nchini Machi 21.

Kwa mujibu wa Msangi, bingwa wa pambano hilo atakata tiketi ya kwenda kuzichapa kwenye pambano la mabondia nguli duniani, Floyd Myweather na Manny Paqiao litakalofanyika Mei 2 jijini Las Vegas.

"Mbali na pambano hilo pia mabondia Mada Maugo atazichapa na Japhet Kaseba kwenye uzani wa super middle na Thomas Mashali atazichapa na Karama Nyilawila.

Wakizungumzia maandalizi yao, Matumla Jr, Kaseba na Nyilawila walisema wako fiti na kuwataka mashabiki wao kujitokeza kwa wingi  kushuhudia.

Wakati bingwa wazamani wa dunia wa WBU, Rashid Matumla ambaye ni baba na kocha wa mwanae, Matumla Jr akitamba kuwa anaamini mwanae hawezi kumwangusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...