Na Mwandishi Maalum,  New York
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban  Ki Moon  amemteua Jaji Mkuu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Mohamed Chande Othman (pichani)   kuongoza jopo  huru la wataalam watakaopitia taarifa mpya  kuhusu kifo cha   Bw. Dag  Hammarskjold ambaye  aliwahi kuwa   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
“ Katibu Mkuu anayofuraha ya  kutangaza kwamba amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa   jopo huru la wataalamu. Bw.  Mohamed Chande Othman kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ambaye atakuwa mkuu wa jopo hilo. Wajumbe wengine ni  Bw. Kerryn Macaulay kutoka Australia na Bw.  Henrik Ejrup  Larsen kutoka Denmark” inasomeka taarifa  iliyotolewa   na   Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu
Uteuzi wa Jopo hilo unatokana na Azimio   namba 69/246 la Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa lililopitishwa  tarehe   29 mwezi Desemba  2014  ambalo lilimtaka   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuteua jopo la wataalam huru ili kuchunguza na kutathimin thamani ya taarifa mpya ( probative value)zinazohusiana  na kifo  cha Katibu  Mkuu  Dag Hammarskjold pamoja  na watu waliofuatana naye.
Bw. Dag Hammarskjold na ujumbe wake alipoteza maisha katika ajali ya  ndege iliyotokea mwaka 1961 wakati akitokea  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Baadhi ya  Majukumu ya Jopo hilo huru la wataalamu pamoja na mambo mengine  yatakuwa kupitia na kutathmini thamani ya  taarifa mpya ambazo Kamisheni ya Hammarskjold imeziwasilisha   kwa Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Vile vile  litatathmini   taarifa mbalimbali ambazo zimetolewa na  nchi wanachama na vyanzo vingine.

Jopo hilo la wataalam huru litaanza kazi yake mwisho mwa mwezi huu wa March ( 30 March) na  linatarajiwa  kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu  Mkuu si Zaidi ya  tarehe 30 mwezi June mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...