Mwimbaji wa siku nyingi wa nyimbo za injili
nchini, Jennifer Mgendi, ameachia albamu yake mpya mapema wiki hii.
Akizungumza na blogu hii Mgendi amesema albamu hiyo ina jumla ya
nyimbo saba ambazo ni Wema ni Akiba, Nani kama Mungu?, Nakungoja
aliomshirikisha Mchungaji Abiudi Misholi, Kimbilia Msalabani, Nakuhitaji Roho,
Tenda nishangae na Wastahili.
Akizungumzia video ya albamu hiyo, Mgendi
amesema maandalizi ya video yameanza na video itazinduliwa Juni 28 katika
kanisa la DCT Tabata Shule katika tamasha litakaloambatana na shukurani ya
kutimiza miaka 20 tangu aanze uimbaji.
Mbali na uimbaji Jennifer pia ni muandaaji
wa filamu mbalimbali za kidini hadi sasa akiwa na filamu tano Joto la roho,
Pigo la faraja, Teke la Mama, Chaimoto na Mama Mkwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...