Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala wamefanya ziara katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuona utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) na kukutana na walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini unaotekelezwa na mfuko huo.

Wakizungumza na walengwa hao katika kijiji cha Madabaga wabunge hao wameonyesha kuridhishwa na mafanikio makubwa yaliyoanza kupatikana baada ya walengwa kupata fedha chini ya utaratibu wa uhawilishaji fedha unaotekelezwa na Tasaf.

Wakizungumza katika ziara hiyo baadhi ya walengwa wameeleza namna walivyonufaika na fedha zilizokwishatolewa ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto,kuboresha makazi yao na kuwa na uhakika wa huduma ya afya na lishe.

Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika kijijini Madabaga,mwenyekiti wa kamati hiyo Vedastus Rweyikiza amewahimiza wananchi hao kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu ikiwa ni pamoja na kubuni miradi itakayowafanya wawe katika mazingira mazuri hata baada ya mpango huo kumalizika.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Tasaf Ladslaus Mananga,mkurugenzi wa ukaguzi wa mfuko huo,Christopher Sanga alibainisha kuwa jitihada za kuwafikia walengwa wote wa mpango huo zinaendelea ambapo ifikapo katikati ya mwaka huu zaidi ya kaya milioni moja zitanufaika na utaratibu wa uhawilishaji fedha nchini kote.
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro(wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala kabala ya wajumbe hao kutembelea walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarani mkoani humo.Kulia ni mkurugenzi wa ukaguzi wa Tasaf Christopher Sanga.
 MKuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhussein Kifu(wa nne kulia) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala kabla ya wajumbe hao kutembelea walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarani mkoani humo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na UtawalaVedastus Rweyikiza akizungumza jambo baada ya kamati hiyo kukutana na wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani mkoani Mbeya.
 Wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani mkoani Mbeya wakimsikiliza mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala Vedastus Rweyikiza kabla ya kuanza kugawiwa fedha kwenye mkutano uliofanyika kijijini hapo jana.
 Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani Hellena Bamba akikabidhiwa fedha kutoka kwa kamati ya mradi ya wilaya(CMC).
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala wakiangalia namna wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani wanavyokabidhiwa fedha.Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Vedastus Rweyikiza kushoto kwake akifuatiwa na Felix Mkosamali na Willium Ngeleja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...