Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Kampuni ya East Africa Unique Co.LTD imeandaa semina itakayo anza mwezi April mwaka huu kwa wafanyabiashara juu ya kuwajengea uwezo wenye miradi itakayo kuwa na uaminifu na kujituma kulingana na uwezo pamoja na ukomo wao.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Rodgers Mbaga amesema Kampuni hiyo ambayo inashughulika na ushauri,mawasiliano ya masoko imebuni na kupanga Maonyesho ya Kukuza Uwekezaji-TIPEC kwa lengo la kuweka msukumo zaidi kwenye uwekezaji na hatimaye kuinua uchumi.

Amesema kampuni hiyo imepanga kuwainua wafanyabiashara nchini katika program ambazo wanazifanya kutokana na kukosa mwamko katika fursa za uwekezaji nchini.

Amesema semina hiyo itakuwa na kiingilio cha dola za kimarekani 100 kwa mtu na kushiriki mara moja katika kila jumatano ya mwisho wa mwezi.

Kampuni hiyo inatarajia kufanya gulio Juni 3 hadi 4 mwaka huu na kuweza watu kuandika miradi yao na kwa ajili ya kuwea kupata washirika wa kuendesha mawazo yao zaidi ya miradi 100itakuwapo katika maonyesho hayo na makampuni 100 yatashiriki na gharama za ushiriki dola za kimarekani 1000 na 3000.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya TEPAC Rodgers Mbaga (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu kuwepo kwa mkutano na maonesho ya kukuza uwekezaji yatakayofanyika Juni 3 hadi 5 Mwaka huu. Kushoto ni Meneja miradi wa kampuni hiyo Tony Swaheh na kulia ni Ofisa mwandamizi ukuzaji masoko wa TEPAC Stephen Kobero. Picha na Agnes Alcardo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...