Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Mkoka wakitazama Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake ukikatiza kwenye moja ya daraja wakati wakielekea katika kijiji hicho cha Mkoka,Wilayani Kongwa mkoani Dodoma,Ndugu kinana aliweka jiwe la msingi la kitega uchumi cha tawi la CCM pamoja na kufungua Ofisi ya CCM Tawi la Mkoka.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Mamia ya wakazi wa kijiji cha Mkoka wakishangilia jambo wakati
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara Wilayani Kongwa mkoani Dododoma.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkoka,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.



 sehemu ya umati wa watu wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mkoka,Wilayani Kongwa.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa wamefuatana na wananchi walipokuwa wakiwasili katika uwanja wa Mkoka kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara,mbali ya Uongozi huo wa juu wa CCM,pia waliambatana Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Chiku Galawa,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma,Mh.Addam Kimbisa pamoja na viongozi wengine wa wilaya.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani juu ya jengo akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai wakishiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Njoge,Kata ya Njoge pamoja na kusalimia Wananchi wa eneo hilo.
Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kushiriki ujenzi wa darasa la shule ya msingi Mlali,katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa,mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni mia sita ulianza kujengwa mnamo mwaka 2013 na kutarajiwa kumalizika mei 2014,lakini kwa bahati mbaya mradi huo haukukamilika kwa wakati kutokana na ukosefu wa fedha.Mbunge wa jimbo hilo la Kongwa,Mh.Ndugai alieleza kuwa mradi huo kwa sasa umekwishakamilika kwa asilimia tisini na kwamba mradi huo wa maji safi na salama utawanufaisha wanakijiji wapatao mia saba na zaidi.

PICHA NA MICHUZI JR-WILAYANI KONGWA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...