Mwenyekiti wa Taasisi ya Save Vulnerable, Fredy Kayula (kulia) akimpatia Kiongozi wa kituo hicho, Mchungaji Amani Kayuni, (wa kwanza kushoto) msaada wa nguo, chakula na vifaa vingine kwa watoto wasiojiweza katika kituo cha Yatima Group Trust Fund kilichopo eneo la Chamazi,Mbagala wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watoto wanaolelewa kwenye Kituo cha Watoto Yatima cha Chamazi Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
---
---
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Kituo cha Watoto Yatima cha Chamazi Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, kimesema kinakabiliwa na changamoto ya kulipia karo wanafunzi waliopo elimu ya msingi,Sekindari na Chuo Kikuu na kutaka msaada kwa jamii kuweza kuwasaidia ili waweze kusoma.
Hayo aliyasema Mkuu wa Kituo hicho,Winfrida Lubanza wakati akipokea msaada kutoka Taasisi ya Save Vulnerable Foundation(S.V.F)kwa kushirikiana na Kanisa la EAC lilopo Sinza jijini Dar es Salaam,Winfrida amesema kituo kina miradi mbalimbali wanayoendesha ambayo ni michanga hawawezi kotokana na uchanga huo.
Amesema changamoto zingine ni chakula pamoja na kuweza kupata ukuta katika kituo hicho ambapo msaada mkubwa wanategemea kutoka katika jamii zikiwemo taasisi ,makampuni pamoja na mtu binafsi kutoa msaada katika jamii hiyo iweze kusonga mbele na kufikia malengo yao.
Mwenyekiti wa SVF, Fredy Kajula amesema wataendelea kutoa msaada kwa watu wa jamii hiyo kutokana na program zilizopangwa watoto walio katika mazingira magumu.
Kajula amesema msaada huo nguo ,mchele ,unga wa mahindi pamoja na vifaa vya mashuleni ambavyo vimechangiwa na kanisa pamoja na taasisi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...