Lori la Mizigo lenye namba za usajili T 535 CCT mali ya Kampuni ya Coast Millers Limited watengenezaji wa Unga wa Ngano wa Nyati, likiwa nje ya barabara ya Kawawa eneo la Karume mara baada ya kuigonga Treni ya TRL mapema leo asubuhi.

Sehemu ya mashuhuda wa tukio hilo.
Askari Polisi wakiwa eneo la tukio.
Sasa hili Lori vipi au kosa ni waongoza treni inapovuka barabara, hili swala litafutiwe ufumbuzi lisije kujirudia na kusababisha hasara kubwa zaidi..
ReplyDeleteMadereva wengi wawapo barabarani hawazingatii alama za barabarani na ndiyo inayopelekea ajali nyingi barabarani. Kila siku tunaimba wimbo huohuo sijui lini madereva watatambua umuhimu wa usalama barabarani. Wanajiamini vipi wakati wanaendesha vyombo vya hatari? nashindwa kuelewa kabisa, mbona mimi ni mwoga hata tu kujifunza gari. Da! kweli kazi ipo
ReplyDeleteHizi njia za treni (reli) zinapokutania na barabara za magari zitenganishwe sasa, aidha iwe treni inapita juu gari chini au gari juu treni iwe inapita chini kwa kujenga vidaraja vya kutenganisha
ReplyDeletenina mashaka huyo dereva wa lori alikuwa anasinzia wakati anaendesha...hao wanasomba ngano usiku kucha kutoka bandarini mpaka kiwandani kwao mandela road...hawapumziki hao mpaka ngano wamalize melini...
ReplyDelete