Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unachukua fursa hii kukanusha vikali taarifa
potofu zilizoandikwa na baadhi ya magazeti kuwa mabehewa 22 ya abiria yaliyonunuliwa na
Serikali kutoka Korea ya Kusini ni mabovu. Mabehewa haya yalikwisha fanyiwa majaribio na
TRL kuridhika kuwa hayana kasoro yoyote.
Hoja kuwa tokea yawasili nchini mwezi Desemba , 2014 hayajaanza kutumika kwa vile ni
mabovu ni upotoshaji wa ukweli. Ukweli ni kwamba kuanzia Novemba 24, 2014 TRL ilipeleka
maombi katika Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini –SUMATRA ya
kuruhusiwa kuanzisha huduma ya treni ya abiria ya “deluxe’ kwa kutumia mabehewa hayo na
kutoza nauli maalum.
Februriari 25, 2015 Sumatra imetoa idhini ya kuanzisha huduma hiyo kwa kuyatumia
mabehewa hayo 22 baada ya kutimiza masharti ya uendeshaji. Hivi sasa TRL inakamilisha
masharti hayo na safari ya kwanza ya uzinduzi inatarajiwa kufanyika Aprili 1, 2015 kwenda
Kigoma kupitia katika stesheni zilizoainishwa katika jedwali la nauli ambalo limekuwa
likitangazwa na baadhi ya magazeti tokea wiki iliyopita.
Kuhusu kadhia ya ubovu wa mabehewa aina mbalimbali yakiwemo yale 25 ya kubebea kokoto
BHB, 50 ya kubebea Makasha CCB, 100 ya kubebea mizigo ya kichele CLB na 17 ya breki BVB
haya yote yamenunuliwa kwa mikataba maalum ambayo imeweka masharti kwa gharama za
mtengenezaji kuyafanyia marekebisho endapo hitilafu zitajitokeza wakati kipindi cha majaribio.
Aidha mikataba yote imetoa dhamana ya kati ya mwaka mmoja na miwili kwa ajili kurekebisha
hitalafu zozote zitakazojitokeza wakati wa matumizi ya vitendea kazi hivyo.
Kwa taarifa hii tunawaomba tunawahakikishia wananchi wote kuwa mabehewa ya abiria
yailyotengenezwa nchini Korea Kusini ni ya viwango vy ahalio ya juu. Abirfia wanaosubiri kwa
hamu kuanza kwa safari za ‘ Deluxe Train’ wajiandae kusafiri kwa raha na wavipuuze vyombo
vya habari ambavyo kwa makusudi vinapotosha umma.
Karibuni tupande treni ya Deluxe kwenda Kigoma Aprili 01 , 2015 tuone ukweli halisi.
Imetolewa na
Afisi ya Uhusiano wa TRL kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji , Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu Dar es Salaam, Machi 11, 2015
Imetolewa na
Afisi ya Uhusiano wa TRL kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji , Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu Dar es Salaam, Machi 11, 2015
Of all the dates kwqa nini ianze tarehe 1 April 2015 na wala si nyingine?
ReplyDelete