Na  Bashir  Yakub.

Kumekuwa  na  shida  sana  hasa  kwa  upande  wa  wanaume  kuwatelekeza  watoto. Mara  nyingi  wanaume  ndio   hutelekeza  watoto  kuliko  wanawake. Zipo  baadhi  ya  kesi  zimeripotiwa  zikihusisha  wanawake  kuwatelekeza  watoto   lakini hizi  si  nyingi  kama  ilivyo  kwa  wanaume. Hii  ni kwasababu  uwezekano  wa  mwanaume  kumkimbia  mtoto  ni  mwepesi  kuliko mwanamke  kumkimbia  mtoto/watoto.  Jambo  hili  ni  baya  na  limeshakemewa  na  sheria  mbalimbali.  Nataka   niwaeleza  kuwa  kumtelekeza mtoto   ni  kosa  la  jinai. 

Nikisema ni  kosa  la  jinai   maana  yake  ni kuwa  kulifanya  kwake  kunahitaji   adhabu  ya  kifungo  jela au adhabu  nyinginezo. Wapo watu  hasa  wanawake  ambao  wamekuwa  wakitupiwa  watoto  na  wanaume  kwa makusudi.  Ni  ushauri  wangu  kwamba  muda  ni huu  sasa kama  ulikuwa  hujui  kuanzia  leo  ujue  na  uchukue  hatua. 

1.NINI  MAANA  YA  KUTELEKEZA  WATOTO/MTOTO  KISHERIA.

Kutelekeza mtoto/watoto   ni  pamoja  na  kutotoa  matumizi  kama  chakula, mavazi , matibabu, makazi,  na  mahitaji  ya  msingi( necessity) kama  ada  za shule, vifaa  vya  shule  na  kila  kitu  ambacho  ni mahitaji  ya  msingi  kwa  makuzi  na ustawi  wa  mtoto.  Kwa hiyo  mzazi  asiyejihusisha  kwa  namna  yoyote  na  huduma  hizi  nilizotaja kwa  mujibu  wa sheria  huyu  ndiye  aliyetelekeza  mtoto/watoto.

2.KUTELEKEZA  WATOTO/MTOTO  NI  KOSA  LA  JINAI.

Sura  ya  16  Sheria  ya Kanuni  ya  Adhabu  kifungu cha  166  kinasema  kuwa  Mtu yeyote ambaye, ni  mzazi  au  mlezi  au mtu  mwingine  mwenye  uangalizi    halali  wa mtoto  yeyote  mwenye  umri  usiozidi  miaka   kumi na nne, hali  ana  uwezo, wakumuhudumia  mtoto, kwa  kuamua  au kinyume  cha sheria, au  bila ya sababu za msingi akakataa  kumhudumia, na akamtelekeza  mtoto  bila  msaada, atakuwa  ametenda kosa. Kwahiyo  kumbe  kutokana  na  sheria  hiyo  kumtelekeza  mtoto   ni  kosa  la  jinai  kama  zilivyo  jinai  nyingine  kama  kuiba, kuua , kubaka n.k.
Aidha  ni muhimu  walioarhirika  na  matendo  ya  kutupiwa  watoto  wachukue  hatua  za  kufungua  kesi  za  jinai  ili  wahusika  wawajibishwe.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Thubutu, sio wanaume wa Kitanzania hawatoi matunzo wala huwezi kuwapeleka mahakamani. Tuliona kesi ya IGP wa zamani aliyepelekwa mahakamani matokeo yake ilikuwaje?

    ReplyDelete
  2. Serekali ya siku hizi! Wanawake wengi maskini wamejichokea! Kila wanachojaribu wale wanaue wanaenda kuhonga na kuwatishia! nafikiri wengi wao wanasubiri tu Ukombozi wa Masia na sio serekali ya vyombo vyetu vya dola! Nothing called laws are enforced in Tanzania and if they are, is for the poor men who can not bribe and play the corruption crap!
    Mahousegirl walopewa mimba na kufukuzwa na watoto wao wako wapi? Walopewa mimba za bila mipango wako wapi???

    ReplyDelete
  3. nDUGU YAKUBU, HEBU TUPE UFAFANUZI KUHUSU KUMTUNZA MTOTO, NILIFIKIRI KUMTUNZA MTOTO NI JUHUDI ZINAZOUNGANISHWA NA PANDE MBILI YAANI MWANAUME NA MWANAMKE, LAKINI KATIKA MAKALA YAKO INAONEKANA KAMA MWANAMKE AHUSIKI KATIKA GHARAMA KAMA MALAZI, MAVAZI NA HATA CHAKULA, NAOMBA UFAFANUZI HAPO.
    MBEGU

    ReplyDelete
  4. Hii sheria inafahamika kwa wale wachache wenye mwanga kidogo wa mambo ya sharia. Lakini wale ambao wako tayari kutoa ada ya tunzo ya motto kwa mwezi nikiasi gani? je inakidhi mahitaji ya mtoto kutokana na maisha ya sasa? Hili ni jambo la kuliangalia kwa undani. Nchi kama Botswana ukipitisha mwezi mmoja hujalipa wakiripoti utakwenda ndani,haijalishi cheo wala umaarufu wa mtu.

    ReplyDelete
  5. Wewe bwana mbegu unataka ufafanuzi! Anasema wanaume wengi wamewateketeza watoto wao! Hawajui wanakula nini wanavaa nini wala wanasoma nini au wapi? SItaki kuleza zaidi lakni mimi ni mwanaume na nimeshudia marafiki zangu kiabo wao kueana mimba na binti sio ishu ila ishu ni binti akisema ana mimba atatukanwa, kupigwa na kudalilishwa kwa kila aina hapo anakata awasiliano kabisa! Sasa hao watoto mwenzetu aloacha huko barabarani nani anawalea! Mama zao kivipi? hajui wala haijulikani!?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...