Na  Bashir  Yakub.

Kumekuwepo  na utata  mkubwa  kuhusu  urithi  wa  mali  za  marehemu  hasa  inapotokea  kuwa  marehemu  alikuwa  na  mke   zaidi  ya mmoja  na  hapohapo  watoto  wanaotokana  na  mama  tofauti.  
Tumeshashuhudia  magomvi  makubwa  misibani   lakini  pia  tumeshuhudia  na  tunaendelea kushuhudia  utitiri  wa mashauri  kuhusu  mkanganyiko  wa  mali za marehemu ambaye  familia  yake  ni  ya watoto  wanatokana  na  mama  tofauti. 
Kutokana  na  hayo  kuna umuhimu  mkubwa  wa kueleza sheria  inasemaje  kuhusu  mazingira  ya  namna  hiyo ili  anayemua kuchukua  hatua  au  kulalamika  alalamikie  kitu  ambacho  ni  haki  yake  kweli na  anayeamua  kuacha  aache  akiwa  ameridhika  kuwa  hajaonewa  isipokuwa  hicho  alichopata  ndiyo  haki   yake  kisheria. 

1.NINI  MAANA YA MKE  WA  NJE  YA  NDOA.

Mke  wa  nje  ya  ndoa  ni  mke  ambaye  ameishi  na  mume  kama  mke  na  mume  lakini  akiwa  hajafunga  ndoa  yoyote  ya  kiislamu, ya  kanisani, ya  serikali au  ya kimila. Ndoa  ya kiislamu hufungwa  kwa taratibu  za kiislamu  ambazo huhusisha  masheikh, makadhi n.k. Ndoa  ya  kikiristo  hufungiwa  kanisani  na  yaweza  kufungishwa  na  mchungaji, askofu, padre n.k. Ndoa ya  serikali  hufungwa  katika  mamlaka  za serikali  kama  kwa mkuu wa wilaya  ubalozini n.k. Na  ndoa  za kimila  ni  ndoa  ambazo  hufungwa  kutokana  na mila  na  desturi  za jamii  fulani kwa mfano  ndoa  za kihaya, ndoa  za kichaga n.k. Kwa hiyo  kama  mwanamke  hana  ndoa  yoyote  katika  hizi  basi  yeye  ni  mke  wa  nje  ya ndoa.

2. NINI  MAANA YA  MTOTO  WA  NJE  YA NDOA.

Mtoto  wa  nje  ya  ndoa ni mtoto aliyetokana  na  ndoa  isiyohalali au  mahusiano  yasiyo  halali. Hapo juu  nimetaja  aina  za ndoa halali. Hii ina  maana  kuwa  iwapo  mtoto  amepatikana  nje  ya  ndoa  hizo  basi  huyo  ndiye  anayeitwa  mtoto   wa nje  ya  ndoa. 

3.  MKE    ASIYE  NA  NDOA  HARITHI.

Kwa  mujibu  wa sheria  zetu  hapa  Tanzania  zikiwemo   tafsiri  mbalimbali  za  sheria  hizo  ambazo  hutolewa  na  mahakama  kuu pamoja  na  mahakama  ya  rufaa  mke wa  wa  nje  ya  ndoa  hutambulika  kama  kimada. Neno  kimada  sio  tusi  isipokuwa  ni  neno  la  kitaalam  linalomwakilisha  mwanamke  anayeishi  na  mwanaume  bila  ndoa  na  ndio  maana  neno  hilihili  limetumiwa  na  mahakama  katika  hukumu  zake  mbalimbali. 

BOFYA HAPA Kusoma zaidi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sasa ndugu Bashir mbona unanichanganya, juzijuzi uliandika kwamba watu walili wakikaa pamoja kama mume na mke kwa miaka miwili basi hii ni ndoda halali hata kama hawajafunga ndoa kanisani, msikitini, serikalini au kijadi (cap 160). Sasa tuamini ipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...