Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere leo amezungumza na waandishi wa habari,nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam juu ya uvumi ulioenea nchini kuwa amefariki Dunia.


Mama Maria amewathibitishia watanzania kuwa bado yu hai na mwenye nguvu hivyo wasiwe na hofu nae. Alisema jana amepokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto zake, wake wa watoto zake wote, familia yake pamoja na watu mbalimbali ili kumjulia hali.

Amesema alipopokea taarifa hizo wala hakushtushwa badala yake alifanya sara kwani uvumi huo wawezekana inatokana na vuguvugu la uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, pia utandawazi uliopo wa sayansi na teknolojia wa karne ya 21.

"jana nilipokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto wangu, wake wa watoto zangu, pamoja na familia,walikuwa wakinisalimia, wengine waliposikia sauti yangu walikata simu" alisema Mama Maria.

Mama Maria alisema taarifa hizi za kuzushiwa kifo si mara ya kwanza kwani hata miaka ya nyuma akiwa na hayati baba wa Taifa, mwalimu Julius Nyerere walipokea taarifa nyingi za uvumi wa kifo.

Mjane wa hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam leo,juu ya uvumi wa kufariki Dunia ulioenea jana kupitia simu na mitandao ya kijamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. The mdudu, haya naomba uchunguzi haraka sn na kama hamuwezi kufanya hiyo kazi basi wakabiziwe jwtz na hakuna atakaejificha kisha tuwafunge maisha because hawafai kuwepo kwenye hii dunia ili iwe fundisho kwa wajinga kama hao.

    ReplyDelete
  2. SHETANI NA ASHINDWE KATIKA JINA LA YESU, MAMA YETU NA AISHI MAISHA MAREFU ZAIDI.

    ReplyDelete
  3. Mungu akubariki Mama Maria

    ReplyDelete
  4. pole mama kwa kuzushiwa...ila wote sie ni maiti zinazotembea... accept

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...