Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Binilith Mahenge ameishauri Halmashauri ya Jiji la Mbeya kutafuta wawekezaji watakaotumia taka kama malighafi katika shughuli uzalishaji viwandani ili kukabiliana na uchafuzi wa mazingira jijini humo.

Ushauri huo aliutoa, akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo wakati alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya na kuzungumza na Idara ya Usafishaji na Mazingira jiji humo jana.

Aliongeza kusema kuwa taka ni mali, zinaweza kutumika katika uzalishaji wa bidhaa nyingine huku akitolea mfano Kiwanda cha Falcon, kinachozalisha milango pamoja na chemba za vyoo kwa kutumia taka huko jijini Mwanza.

Pia katika ziara hiyo Mh. Mahenge, alitembelea Mtaa wa Ntungi, Kata ya Nsalaga ili kuona ujenzi wa dampo jipya lenye mita za ujazo 454,000, linaloweza kutumika ndani ya miaka sita ambalo ujenzi wake umewezeshwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi bilioni 3.8.

Wakati huo huo pia, alitembelea hifadhi ya Safu ya Mlima Mbeya ili kujionea mikakati ya utunzaji mazingira inayotekelezwa katika hifadhi hiyo, ikiwemo upandaji miti kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji pamoja na ugawaji wa mbegu ya miti ya kuni bure kwa wananchi waishio karibu na hifadhi ili kuhepusha vitendo vya ukataji miti katika hifadhi hiyo.

Katika majumuisho ya ziara yake mkoani Mbeya, Mh. Mahenge alitembelea kiwanda cha saruji cha Mbeya Ciment, ambapo aliridhishwa na uendeshwaji wa shughuli za uzalishaji kiwandani hapo nakuupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuzingatia Kanuni za Mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Binilith Mahenge (katikati), akitoa majumuisho wakati akimalizia Ziara yake ya Siku mbili iliyofanyika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya nakumalizikia katika Kiwanda cha Saruji kilichopo eneo la Songwe, Mkoani humo jana. (Picha na OMR)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Saruji ipungue bei Mbeya, kiwanda kipo kwetu saruji wanatuuzia bei sana tofauti na mikoa mingine. Mfuko mmoja 16,000 wakati Dar 14, 000 sijui kipi tofauti wanatungonga sana Mbeya jamani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...