Waziri wa Uchukuzi Mhe Samuel Sitta akifunga mafunzo ya waendesha boda boda chuo cha FDC wilaya Urambo leo. Katika nasaha zake, Mhe Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo la Urambo, amewataka waendesha Bodabod hao kuzingatia mafunzo walioyapata kwa makini ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika. Aidha, ametoa wito kwa vijana hao kuwahamasisha wenzao kushiriki katika mafunzo ya aina hiyo na pia kujiendeleza na kozi nyingine za ufundi pale zinapobidi. Mhe Sitta aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kufu nga mafunzo hayo, ametoa vyeti kwa wahitimu wa chuo hicho wapatao 63
Waziri wa Uchukuzi Mhe Samuel Sitta akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu 63 wa kozi hiyo mafunzo ya waendesha boda boda chuo cha FDC wilaya Urambo leo.
Waziri wa Uchukuzi Mhe Samuel Sitta akijiandaa kupandisha bendera wakati wa uzinduzi wa Tawi la vijana wa CCM wilaya ya Urambo mjini leo
Waziri wa Uchukuzi Mhe Samuel Sitta akipandisha bendera ya CCM katika uzinduzi wa Tawi la vijana wa CCM wilaya ya Urambo mjini leo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...