Hatimaye wakurugenzi wa Mashauzi Classic na Jahazi Modern Taarab, wamefanya mkutano na waandishi wa habari na kuthibitisha kuwepo kwa onyesho la pamoja la makundi hayo yenye nguvu katika muziki wa taarab.
Onyesho hilo litafanyika mwezi huu Jumapili tarehe 22 ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni.
Mkurugenzi wa Jahazi, Mzee Yussuf na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhan maarufu kama Isha Mashauzi, wamesema siku hiyo hatumwi mtoto dukani.
Wakiongea katika mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika Jumatatu jioni katika hotel ya Travertine Hotel, wakurugenzi hao ambao wote ni waimbaji nyota, wakasema onyesho hilo si mpambano lakini pia sio la masihara kwani kila bendi imejipanga kuhakikisha inaangusha burudani iliyokwenda shule.
Kutoka
kushoto ni Meneja wa Mashauzi Classic Ismail Rashid, Isha
Mashauzi, Mzee Yussuf na Seif Magwaru meneja wa Jahazi Modern Taarab.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...