Benki ya NMB hivi karibuni imezindua matawi mapya mawili yaliyopo kwenye mikoa ya Tabora na Shinyanga. Hii ni habari njema kwa wakazi wa maeneo hayo na kwa wateja wa benki ya NMB kwa ujumla ambapo awali walitembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma za kibenki. 
 Kuongeza matawi hayo yanamaanisha NMB imewafikia wateja wake katika kila wilaya nchini. Uzinduzi wa matawi hayo NMB Kaliua na NMB Kishapu yamezidi kuongeza idadi ya matawi ya NMB yaliyotapakaa nchi nzima kuwa zaidi ya 170. 
 Tawi la NMB Kaliua liko karibu na kutuo cha reli cha Kaliua wakati tawi la Kishapu lipo umbali wa kilometa 49 kutoka barabara ya Shinyanga – Mwanhuzi kutoka Urambo. Tembelea matawi haya ufurahie huduma na bidhaa mbalimbali zitolewazo na benki yako ya NMB.
Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi - Bw. Abraham Augustino (kushoto) akishangilia pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga - Mhe. Ally Rufunga baada ya kufungua pazia kuashuria ufugunguzi rasmi wa tawi la NMB Kishapu.
                                     Tawi la NMB Kishapu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...