Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakimjulia hali Meja Peter Lyamuya aliyelazwa katika hospitali kuu ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam akiuguza jeraha la mguu alilopata baada ya ndege ya kivita aliyokuwa akiiendesha kuanguka na kulipuka wiki iliyopita.Askari huyo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) alinusurika kifo baada ya kufanikiwa kujiokoa katika ajali hiyo iliyosababishwa na ndege mnyama kuingia kwenye injini na kusababisha hitilafu iliyopelekea kushika moto, kuanguka na kulipuka.Ndege hiyo ilikuwa katika mazoezi ya kawaida kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza.(picha na Freddy Maro).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Lugha vipi hapa.Mimi ningependelea ndege pori badala ya ndege mnyama. Na siye tulipokuwa wadogo hiyo ndege nyingine ni ndege ya kivita na zote nyingine ni ndege ulaya.Ankal waulize wataalam watuelimishe.

    ReplyDelete
  2. Sijui lini Watu wa Marekani watatuletea rangi tupake kuta za hospitali yetu.

    ReplyDelete
  3. Mimi nasema na atakae chukia achukie, Rais Kikwete ni Rais bora kuliko wote, ana moyo wa kibinadamu wa kuwajari na kuwapenda wote mdogo na mkubwa, mwenye nacho na hasiye na kitu! Hakika Mh JK ni mtu wa pekee laiti angekuwa mtu mwingine fulani ndie Rais basi tusingemuona kwenye misiba, kuwafariji watu wala kuwapenda watoto, nk!

    Kikwete ndio chagua langu, Kikwete ndie Rais wa Watanzania.

    Mungu akubariki saaana Rais wetu, akupe afya bora na njema maisha yako yoote!

    ReplyDelete
  4. Rangi zimejaa madukani watendaji hospitali ya Lugalo hebu pitisha rangi katika hizo kuta.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...