MUIMBAJI nguli wa Kimataifa wa nyimbo za Injili, Rebecca Malope anatarajia kuwasili Jumaosi ya Aprili 4 akitokea Afrika Kusini kwa lengo la kupanda jukwaa la maadhimisho ya miaka 15 ya Tamasha la Pasaka.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo imekamilika kwa kiasi kikubwa hivyo mashabiki wa muziki wa injili  hapa nchini kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo ambalo litakuwa ni la aina yake.

Msama alisema mwimbaji mwenzake raia wa Afrika Kusini naye pia anatarajia kuwasili Jumamosi akitokea Afrika Kusini na kundi lake ambalo litatoa burudani kwa wakazi wa Dar es Salaam.Msama alisema Muingereza Ifeanyi Kelechi na Eiphraim Sekeleti wanatarajia siku moja kabla ya kuwasili Malope na Mahlangu.

“Tamasha la mwaka huu lina mambo mengi ambayo yataendana na miaka 15 ya tamasha hilo kubwa hapa Tanzania kwa sababu linashirikisha waimbaji wa Kimataifa na viongozi wakubwa serikalini ambao hufikisha ujumbe wa serikali na neno la Mungu pia,”alisema Msama.

Msama alisema muimbaji Mtanzania anyeishi Kenya Faustine Munishi anatarajia kuwasili Aprili 3 kwa lengo la kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu  kupitia waimbaji na viongozi wa dini watakaojitokeza uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hawa wanamuimbia Mungu hawaji kutoa Burudani!!!!???? Kulikoni? Hebu tuheshimu kazi ya Mungu jamani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...