BENDI ya muziki wa dansi hapa nchini,Mashujaa Band 'Wana Kibega' leo imemtangaza Aliyekuwa mwanamuziki na mtunzi
wa bendi ya Ruvu Stars, Rogert Hegga 'Katapila' kujiunga
rasmi katika bendi hiyo.
Mkurugenzi wa bendi ya Mashujaa, Maximilian Luhanga,
alisema kuwa Hegga amejiunga rasmi na bendi hiyo na
watamtambulisha katika onyesho maalumu litakalofanyika
Aprili 5.
Luhanga alisema kwamba kujiunga kwa msanii huyo ni moja
ya mikakati ya kuiimarisha Mashujaa ili iweze kuwa bendi
bora hapa nchini kama ilivyoweza kung'aa kwenye tamasha
la tuzo za muziki la Kilimanjaro.
Alisema kuwa ujio wa msanii huyo utaongeza changamoto
kwenye bendi yao ambayo imelenga kufanya vizuri zaidi
kwenye safu ya muziki wa dansi hapa nchini.
Hegga alisema kwamba ameamua kujiunga na Mashujaa
kwa sababu anataka kufanya kazi katika bendi yenye
wasanii wenye uwezo ambao watatumia vipaji vyao
kuwafurahisha mashabiki wao.
Aliahidi kutowaangusha mashabiki wa bendi hiyo na
mashabiki wake binafsi ambao wanakubali uwezo alionao
kwenye sanaa hiyo.
"Nimekuja kuongeza chachu, nimejiunga Mashujaa kwa
sababu nafahamu wasanii walioko kwenye bendi hii ni bora,
naahidi kuwapa furaha na raha mashabiki wa bendi hii,
hawatajutia ujio wangu ndani ya Mashujaa", alisema
mwanamuziki huyo ambaye amewahi pia kufanya kazi
katika bendi ya Mchinga Sound na African Stars 'Twanga
Pepeta'.
Akizungumzia ujio wa mwanamuziki huyo Rais wa bendi
hiyo Charles Gabriel 'Chalz Baba Kingunge' alisema
kwamba amefurahia ujio wa Hegga ambaye anamuamini na
kuufahamu uwezo wake wa kazi.
Alisema kwamba ushirikiano atakaouonyesha yeye na
Hegga utasaidia kuinyanyua bendi na kuendelea kutamba
hapa nchini.
"Moyo wangu umejaa furaha, nasema karibu sana
Mashujaa, najua uwezo wangu na wako utatoa matunda
mazuri na yenye kulifunuka jiji", aliongeza Chalz.
Moja ya nyimbo ambazo zilipata umaarufu na kutamba
zilizotungwa na Hegga ni Fadhila kwa Wazazi ambayo
aliiandaa akiwa na Twanga Pepeta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...