Na. Johary Kachwamba – MAELEZO, DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetangaza ugunduzi wa gesi asilia katika Miamba ya Mchanga kwenye kisima kinachochimbwa na Statoil cha Mdalasini-1 kwenye bahari kuu ya Tanzania.

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene amebainisha hayo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma. Baada ya kuthibitishwa na Makamu wa Rais wa Statoil, Nick Maden pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

“ugunduzi huo wa gesi asilia wa futi za ujazo trilioni 1.0-1.8, unaongeza kiwango cha gesi asilia iliyopatikana kwenye kitalu namba 2 kufikia futi za ujazo trilioni 22. Kisima cha Mdalasini -1 kimechimbwa katika urefu wa mita za maji ya bahari 2,296 kusini mwa kitalu namba 2” alisema Mhe. Simbachawene.

“kuanzia mwanzo wa uchimbaji, Februari 2012, tumechimba visima 13 na tumefanya ugunduzi katika visima 8 ikiwemo Mdalasini-1. Bado tunaona uwezekano wa gesi zaidi katika eneo la Kitalu namba 2” aliongezea Mhe. Simbachawene

Statoil ni Mkandalasi katika Leseni ya Utafutaji ya Kitalu namba 2 kwa niaba ya TPDC na inayohisa ya asilimia 65% na mshirika wake ExxonMobil and Production Tanzania Limited inazo hisa asilimia 35%.

Wakati wa uendeshaji baada ya Serikali kutoa Leseni ya uzalishaji, TPDC kulingana na mkataba inaweza kushiriki katika uendeshaji na uzalishaji kwa kutwaa asilimia 10% ya uwekezaji.
Waziri wa Nishati na Madini (wa pili Kulia) Mhe.George Simbachawene akizungumza na waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu Ugunduzi wa nane wa gesi asilia uliyofanywa na Kampuni ya Statoil katika eneo la Bahari Kuu,(wa kwanza kulia) ni Naibu Waziri Nishati na Madini Dkt Charles Mwijage,na (wa kwanza kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Nishati na Madini Mhe.Richard Ndassa (Mb) wa Sumve CCM. Picha na Anitha Jonas-MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ugunduzi huu wa gesi asilia ni baraka kubwa kwa nchi yetu..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...