TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo imepongezwa na serikali kwa hatua yake ya kufungua tawi wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Meneja Mauzo wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, akimuelekeza jambo Katibu Tawala wa Wilaya Kwimba, Vicent Emmanuel, katika uzinduzi wa tawi jipya wilayani humo, uliofanyika Machi 2 mwaka huu. Wengine ni maofisa wa taasisi hiyo, Ramadhan Hanafi na Monica Mwangoka. Picha na Mpigapicha Wetu.

Shughuli za uzinduzi huo zilifanyika Machi 2 mwaka huu, huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, akiongozana na viongozi mbalimbali wa serikali wilayani humo.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, kushoto akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi tawi jipya la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. Kulia ni Meneja Mauzo wa taasisi hiyo Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Picha na Mpigapicha Wetu.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Tawala huyo wa wilaya Kwimba, Emmanuel alisema kwamba kufunguliwa kwa tawi hilo kutatoa huduma karibu na wananchi, kama njia ya kukuza uchumi wao kwa ujumla, zikiwapo fursa za kukopeshwa bidhaa mbalimbali, vikiwamo vyombo vya usafiri.

Alisema kwamba awali watu wa Kwimba walilazimika kusafiri umbali mrefu kupata huduma za mikopo, lakini sasa wamesogezewa huduma karibu, hivyo ni jukumu lao kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujinufaisha kwa ajili ya maisha yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...