Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Utafiti unaonyesha kuwa magonjwa ya kifua Kikuu , Ukimwi ,Kansa pamoja na ajali zinachangiwa na matumizi ya pombe kwa kiwango cha juu, na vijana ndio waathirika wakubwa kutokana na kutokuwepo kwa sera ya matumizi ya pombe.

Utafiti huo umetolewa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR),uliofanywa katika Mikoa ya Kilimanjaro na Mwanza na ambao ulilenga vijana kuanzia Miaka 15-24.

Wakizungumza katika semina ya wadau wa masula ya afya leo jijini Dar es Salaam ,Watafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR) , wamesema kuwa matumizi ya pombe nchini yako katika kiwango cha juu na kusababisha magonjwa kuchangiwa na matumizi hayo.

Mtafiti wa Sayansi ya Jamii wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR), DK. Haika Osaki amesema katika utafiti wa pombe zilizo kwenye mifuko (Viroba) zinanyweka kwa kiwango cha juu na watumiaji ni vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa magonjwa kutokana na kutumia pombe.

Haika amesema nchi ambazo zinafanana kiuchumi na Tanzania kama Zambia na Malawi wamepiga marufuku uzalishaji wa pombe za Viroba kutokana na kuona madhara ya matumizi ya pombe hiyo ambapo vijana wengi wameona ni pombe zenye urahisi wa bei pamoja na uhifadhi wake.

Naye Mtafiti wa NIMR Mwanza, Dk. Said Kapiga amesema kuwa wamefanya utafiti na kuona madhara ya pombe na ongezeko la wagonjwa ambao wanatokana na matumizi ya pombe pamoja na mabadiliko mengine ya kimaisha.
Mtafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu-Kituo cha Mwanza (NIMR), Dk. Said Kapiga akifafanua jambo wakati akitoa mada yake ya ufatiti wa Pombe,katika semina ya Wadau iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mtafiti wa Sayansi ya Jamii wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR) ,DK. Haika Osaki akitoa maada juu matumizi ya Pombe za Viroba katika semina ya wadau iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mshauri wa masuaya Afya na Familia, Dk. Ali Nzige akitoa mada katika semina ya wadau juu madhara ya pombe,kwenye semina iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...