Marafiki wa Wafanye Watabasamu Jumamosi iliyopita waliwatembelea tena watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, ambapo waliwapa zawadi mbali mbali kisha kuchora nao ikiwa ni sehemu ya sanaa tiba (art therapy). 
 Akizungumza na blogu hii, mratibu wa programu hiyo ambaye pia ni mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala, alisema, ziara hiyo iliyokuwa na lengo la kutumia sanaa tiba kukabiliana na msongo wa mawazo, kusahaulisha maumivu na kuwapa nafasi watoto waweze kufanya shughuli walizokuwa wakifanya majumbani. 
Ziara hiyo imewezekana kutokana na michango ya marafiki wa ndani na nje ya nchi ambao walichangia fedha na vitu mbali zikiwamo sabuni, dawa za meno, miswaki, mafuta ya kupakaa, toilet papers, matunda, vifaa vya kuchorea nk. “Tiba sanaa ni sanaa mpya nchini, baadhi ya nchi inatumika mahospitalini, magerezani, makambi ya wakimbizi, mashuleni, kwenye vituo vya kulelea watoto wenye mazingira magumu, majumbani nk. Si kwa watoto tu hata watu wazima inawahusu pia,” Alisema Mpangala. 
 Mpangala alisema programu hiyo imepokelewa vizuri na watoto hospitalini hapo na inaratibiwa kupitia mitandao ya kijamii. 
Kwa watakaopenda kuungana na programu hii watembelee ukurasa wa Wafanye Watabasamu katika facebook. 
 Mpangala amewashukuru, wasanii wenzake, marafiki wa Wafanye Watabasamu, Hospitali ya Taifa Muhimbili, ndugu jamaa na marafiki kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika. Pia vyombo vya habari kwa kupaza sauti za watoto hao.
 Mratibu wa programu ya Wafanye Watabasamu na mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala, akimwonesha mtoto Maurine jinsi ya kuchora katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita. Mpangala na wenzake walitembelea watoto wanaotibiwa saratani ili kuchora nao na kuwapa zawadi mbalimbali. Zaidi kuhusu programu hii tembelea: https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu
 Nguvu ya sanaa tiba kama inavyooneshwa na Clara.
 Sanaa tiba ikawasahaulisha maumivu, wakajihisi wako nyumbani. Baadhi ya watoto wakijiachia na marafiki wa Wafanye Watabasamu waliokwenda kuwatabasamisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita.
 Mtoto Nico akienda sambamba na marafiki wa Wafanye Watabasamu. Kutoka kulia ni Sia Marupa, Masoud Junior na Cloud Chatanda.
 Ha ha ha haaaaaa. Hili ndilo lengo hasa la Wafanye Watabasamu. Mungu akupe nafuu ya mapema Nico. 
Picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...