Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema tukio la kwanza limetokea tarehe 08/03/2015 Majira ya saa 11:00hrs huko  katika kijiji cha Mundemu  Kata ya  Mundemu  Wilaya ya  Bahi Mkoa  wa  Dodoma  mtu aliyefahamika kwa jina la LEGANGA  KAZIMOTO, Mwenye miaka  40, Mkulima na Mkazi wa kijiji cha Mbalawala Manispaa ya Dodoma aliuwawa kwa kupigwa na kitu kizito  sehemu mbali mbali  za mwili wake  na kusababisha kifo chake na watu waliojichukulia sheria mikononi.

Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wizi wa mifugo, kwani marehemu alikuwa anatuhumiwa kuiba ng’ombe mmoja kwa mtu aliyefahamika kwa jina la KENETH NGOSI.

Kamanda MISIME amefafanua kuwa katika tukio hilo watu wanne  wanashikiliwa na Polisi kuhusiana na mauaji hayo akiwemo mwenye ng’ombe huyo ambaye ni KENETH NGOSI Mwenye miaka 48, JOHN  CHINYELA Mwenye miaka 42, Mwingine ni MWESIGA  MASILA Mwenye miaka 30, na JOSEPH  S/O NDALU, Mwenye miaka 38 wote wakulima na wakazi wa kijiji cha Mundemu Wilayani Bahi Mkoani Dodoma.

Aidha Kamanda MISIME amesema tukio lingine limetokea tarehe 08/03/2015 majira ya saa 14:00hrs huko katika kijiji cha Chiwe, Tarafa ya  Mlali  Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma ambapo watoto waliofahamika kwa majina ya MICHAEL SEGUMU, Mwenye miaka 13, Mwanafunzi shule ya  Msingi Chiwe na mwenzake ELIA NGIRA , Mwenye miaka 14, Mwanafunzi shule ya msingi  Msinde wote wa darasa la nne walizama maji na kufa wakiwa wananywesha ng’ombe maji  kwenye korongo lililojaa maji ya mvua.

Chanzo cha tukio hilo ni kwamba watoto hao walikuwa wamesimama juu ya mwamba na ndipo udongo ukamomonyoka na kusababisha wao kutumbukia ndani ya maji yaliyotuama na kufariki dunia.

Kamanda MISIME ametoa wito kwa wananchi waache kujichukulia sheria mkononi kwani ni kosa la jinai na yeyote yule anayejichukulia sheria mkononi polisi hawatasita kumkamata na kumfikisha mahakamani kama hawa waliofanya mauaji haya. Vilevile amewatahadharisha wazazi kuwaangalia watoto wao hasa wakati mvua zinaponyesha kuna madibwi ambapo maji yanatuama na watoto wengi huwa wanapenda kwenda kuogelea hivyo hunasa kwenye tope na kupelekea vifo vyao, hivyo wazazi wanapaswa kuwakataza watoto wanapowaona wanaogelea katika madimbwi ili kuepusha vifo vya nanma hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...