Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Stephen Masatu Wasira amefanya
mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe Mark Childress
ofisini kwake.
Mhe Wasira katika mazungumzo yake na Balozi Childdress alibainisha
changamoto zinazokabili kilimo nchini kuwa ni pamoja na zana duni
zinazotumiwa na wakulima wadogo katika kilimo kuwa ni jembe la mkono.
Alisema kwa kutumia jembe la mkono itakuwa ni ngumu kuondoa umaskini kwa
wakulima wadogo katika maeneo ya vijijini.
Aliongeza kuwa jembe la mkono hutumiwa wakulima wengi wa vijijini katika
uzalishaji wa mazao katika Taifa letu.
’’ Wakulima wadogo ndio tegemeo kubwa katika kuzalisha kilimo hapa nchini
karibu asilimia 90 ya chakula hapa nchini inazalishwa na wakulima wadogo”
alifahamisha Mhe Wasira katika mazungumzo yake.
Soko nalo ni tatizo lingine linalokabili mazao ya wakulima wetu wadogo waishio
vijijini, alitoa mfano wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika mikoa ya Mbeya
na Iringa ambako kuna mazao mengi na hasa mahindi ambayo yamekosa soko.
Pia ameiomba serikali ya Marekani kusaidia kuwekeza zaidi katika viwanda vya
kilimo ili kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wetu ili waweze kufaidika na
juhudi zao na mwishowe waondokane na umasikini
Uwekezaji katika viwanda vya kilimo utasaidia kuepukana na tabia ya kusafirisha
malighafi na hivyo kutaongeza thamani ya mazao ya wakulima wetu, aliongeza
Mhe Wasira.
Aidha, kitu kingine kilichosisitizwa na Mhe Wasira ni mkakati wa serikali
kuwashirikisha vijana katika kilimo ili kuondokana na tabia ya sasa kwa vijana
kukimbilia mjini na hasa Jijini Dar es Salaam kutafuta kile wanachokiita na
kuamini kuwa maisha bora hupatikana mjini.
“ Kilimo cha Bustani ni muhimu kwani kinaweza kuwasaidia vijana kupata kipato
cha haraka kwa kuwa mazao ya aina ya bustani huchukua muda mfupi kupata
mafao yake, “ aliongeza Mhe Wasira.
Mhe. Wasira pia alisema serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inaboresha kilimo
cha umwagiliaji na akaiomba serikali ya Marekani kusaidia katika hili kwani
itaongeza uzalishaji kwa wakulima wadogo kwa kuwa watazalisha mara mbili
kwa msimu mmoja wa kilimo.
Wakulima wanasafirisha mazao ghafi nje ya nchi kama korosho bila kuongezwa
thamani yake na hivi kuwakosesha kupata faida kubwa katika mazao yao.
Naye Mhe Childress aliahidi kuwa serikali ya Marekani itafanyakazi na serikali
ya Tanzania kuhakikisha kuwa inasaidia kilimo hapa nchini.
The mdudu, sasa kama mnalijua hilo la kutokua na zana za kisasa kwenye kilimo kwanini mrikuja na kilimo kwanza? ...ok sawa mm yangu macho the mdudu huyo anaelekea morogoro kugombea ubunge kama mgombea huru nisie na chama.
ReplyDelete